Back to top

(TMA)yakanusha kuwepo kwa kimbunga “Keneth”

22 April 2019
Share

Mamlaka ya hali hewa nchini(TMA)imekanusha baadhi ya taarifa zinazojitokeza katika mitandao ya kijamii zinazodai kutakuwepo kimbunga “Keneth” kuanzia Aprili 26 hapa nchini kikitokea maeneo ya Syschelles na kudai mkandamizo mdogo wa hewa uliopo katika bahari ya Hindi upande wa visiwa vya Madagasca haujafikia kiwango cha kusababisha kimbuka hicho.

Akizungumza na ITV, meneja wa kituo cha utabiri wa hali ya hewa TMA Bw.Samwel Mbuya amesema TMA inaendelea kufuatilia mgandamizo huo unaonekana kuendelea kuimarika katika baadhi ya maeneo ikiwemo katika mwambao wa pwani ya Msumbuji na pwani ya kusini mwa Tanzania katika siku zijazo za juma hili.

Aidha bwana Mbuya amesema kinachojitokeza kwa sasa ni ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo hapa nchini hususani ukanda wa pwani ambayo inasababishwa na ongezeko la msukumo wa upepo katika bahari ya Hindi na kusisitiza TMA itakuwa ikiendelea kutoa taarifa za hali ya hewa kwa kadri mabadiliko yatakavyojitokez