Back to top

TPRI yaanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya viuatilifu.

21 October 2018
Share

Taasisi ya utafiti wa viuatilifu nchini TPRI imeanza kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu hivyo. 

Mpango huo umeanza kutekelezwa kwa wakulima,maafisa ugani pamoja na wataalamu wa wadudu baada ya kugundulika kuwa tatizo sio viuatilifu bali tatizo kubwa ni wakulima wengi kuto kuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi ya viuatilifu hivyo.


Mkuu wa kitengo cha teknolojia za unyunyiziaji wa viuatilifu mhandisi Julias Mkenda anasema mpango huo utasaidia kuondoa changamoto ya  wakulima kukosa mazao ya uhakika kwani watapata uelewa utakao wawezesha kutumia viuatilifu kwa sahihi na kuleta mafanikio.