Back to top

TRA Ruvuma yavuka malengo ya makusanyo ya kodi.

25 January 2021
Share

Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Ruvuma  imevuka lengo la kukusanya kodi kwa kipindi cha julai hadi disemba 2020  kwa kukusanya mapato kwa asilimia 109 na kupewa tuzo ya mkusanyaji bora wa mapato nchini.

.
Kaimu meneja wa  TRA mkoa wa Ruvuma Bi. Amina Ndumbogani amesema tuzo hiyo imekuwa chachu ya kuongeza bidii kwenye ukusanyaji wa kodi na kufanya vizuri zaidi.

.
Kwa upande wake Afisa huduma na elimu kwa mlipa kodi  wa mkoa wa Ruvuma Bw. Justine Katiti amesema baada ya kuwapa elimu wafanyabiashara katika mkoa huo wameelewa kuhusiana na kutumia mashine za kielekroniki kutolea risiti( EFD) na pia kulipa kodi bila shuruti.