Back to top

TRA Tanga yakamata bidhaa zenye thamani ya milioni 572

10 October 2018
Share

Mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamekamata bidhaa mbalimbali kutoka Brazil,Malaysia na Pakistani zilizokuwa zikiingizwa nchini kinyume cha sheria kupitia bandari bubu zilizopo katika wilaya za Tanga,Pangani na Mkinga ambazo zingesababisha hasara kubwa kwa serikali ya kukwepa kulipa ushuru wa zaidi ya shilingi milioni 141.9.
 
Katika zoezi hilo lililoambatana na kuyagawa majahazi matano kwa vikundi vya vya vijana yaliyotaifishwa na serikali baada ya kukutwa yamebeba bidhaa zilizoingizwa kwa magendo,mkuu wa wilaya ya Tanga Bw.Thobias Mwilapwa amewaonya watumiaji kuhakiki ubora wa bidhaa wanazonunua kabla ya matumizi ili kuepuka magonjwa kwa watumiaji.
 
Kufuatia hatua hiyo naibu waziri ofisi ya waziri mkuu,kazi,vijana na ajira Mheshimiwa Anthon Mavunde ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji wa bidhaa haramu kwa sera ya taifa ni kulinda bidhaa za ndani hivyo endapo watashindwa kukabiliana na zoezi hilo ajira za vijana katika viwanda vikiemo vya sukari na mafuta zitafikia ukomo.