Back to top

Trafiki watakaoruhusu magari kujaza abiria kubanwa.

10 May 2020
Share

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw.Aggrey Mwanri amesema serikali itawachukulia hatua, askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani watakaohusika kuyaruhusu magari ya abiria kubeba abiria kupita kiasi na kusababisha msongamano unaokwamisha juhudi za mapambano ya kuenea virusi vya Corona.

Akizungumza na watumishi pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Bw.Mwanri pamoja na mambo mengine amesema licha ya elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kutolewa, lakini bado kumekuwepo na msongamano mkubwa kwenye magari ya abiria hasa yanayo kwenda maeneo ya vijijini.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amewataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yanayotolewa na viongozi wa serikali pamoja na wataalamu wa afya na kuwafichua wale wote wanaokwamisha juhudi za mapamabano ya kuenea kwa virusi vya Corona.