Back to top

TRC ijiendeshe kisasa kukuza uchumi-NDITIYE.

12 September 2018
Share

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amelitaka shirika la reli kutumia mageuzi katika  ya sekta ya usafirishaji kuweza kujiendesha kisasa na kuhakikisha kauli mbiu ya uchumi wa viwanda inatekelezwa kwa ufasaha kupitia uboreshaji wa miundombinu hiyo.

Waziri Nditiye amesema hayo wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika hilo la TRC ikiwa ni katika kuonesha sura mpya ya shirika hilo ambapo amesisitiza kuwa hawatavumilia ujanja ujanja ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya sekta hiyo.

Aidha Waziri Nditiye amewataka wananchi ambao wapo katika maeneo ya hifadhi za reli kuhakikisha wanaondoka katika maeneo hayo.