Back to top

Trump na Kim Jong Un wafanya mazungumzo Singapore

12 June 2018
Share

Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

Marais hao walikutana kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House ambapo wamejadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.

Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ghamu ulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.

Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.

Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.

Akizungumza kabla ta mkutano , katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja wa mataifa utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliono katika mkutano huo.

''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," alisema Guterres.