Back to top

Tuhuma za Rushwa-Watu 8 wakiwemo watumishi 7 TPA kufikishwa Mahakamani

12 June 2020
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, leo Juni 12, 2020 inatarajia kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa 8 wakiwemo 7 wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa tuhuma za Rushwa, Uhujumu Uchumi  na wizi wa zaidi ya shilingi biliomi 8  mali ya TPA.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Afisa Uhusiano(TAKUKURU)  Bi.Doreen inaeleza kuwa kati ya watuhumiwa hao 8, saba ambao walikuwa watumishi wa TPA wameshafukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria na mmoja ni wakili wa kujitegemea ambaye ni miongoni mwa Wakurugenzi wa Mnengele & Associates pamoja na ELA Advocates na hivyo kufanya idadi ya watuhumiwa hao kuwa wanane.

TAKUKURU imesema licha ya kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa hao 8, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini kiasi kingine cha fedha zilizohujumiwa, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuchukua hatua za kisheria kwa watuhumiwa wengine ambao nao wamehusika katika tuhuma hizo ili nao waweze kuunganishwa katika shauri hilo.

Aidha Uchunguzi wa Takukuru umebaini kwamba watuhumi wa hao 8 wamehusika kutenda makosa ya rushwa na uhujumu uchumi jambo lililopelekea upotevu wa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8 mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).