Back to top

Tume ya mawasiliano Uganda yafunga mitandao yote ya kijamii

13 January 2021
Share

Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) Jumanne iliagiza makampuni yanayotoa huduma ya internet kufunga mitandao ya kijamii na app zote za mawasiliano siku mbili tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa UCC, Irene Sewankambo, aliyaandikia barua makampuni hayo, na kuyataka “kuhakikisha kwamba huduma ya mitandao ya kijamii imesitishwa.”

Kufuatia agizo hilo, watumiaji wa mitandao ya kijamii wameripoti visa vya kutoweza kuingia kwenye mitandao kama vile Facebook na Twitter, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda.

Mitandao mingine ni kama vile Viper, Whatsapp na Signal.

VOA