Back to top

Tume ya uchaguzi yaonya waliojipanga kutangaza matokeo ya uchaguzi.

20 October 2020
Share

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa (NEC) Jaji Semistocles Kaijage ameonya vikali taasisi watu au vikundi vya watu waliojipanga kutangaza matokeo ya uchaguzi baada ya zoezi la upigaji wa kura Oktoba 28 kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi anaitoa zikiwa zimebakia siku nane kuelekea katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani na kubainisha jukumu la kutangaza washindi wa uchaguzi ni tume ya taifa pekee na sio vinginevyo.

Kadhalika mwenyekiti huo wa uchaguzi akatangaza zoezi la kuanza kutoa vitambulisho kwa mawakala walioteuliwa na vyama vya siasa kuanzia oktoba 21...insest jaji semistokules kaijage mwenyekiti wa NEC taifa.

Wakati huo huo tume hiyo imesema uchaguzi wa mwaka huu umetumia fedha za ndani na hakuna za msaada wala wafadhili kauli ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasililimali watu NEC Bw. Gerald Mwanulwa wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari na uchaguzi mkuu.