Back to top

Twitter kupunguza wafanyakazi

04 November 2022
Share

Kampuni ya Twitter imewatumia ujumbe wa barua pepe wafanyakazi wake ikiwaarifu kuwa itapunguza wafanyakazi kuanzia siku ya Ijumaa Novemba 04, 2022, ambapo ilibainisha kuwa wafanyakazi ambao ajira zao hazitaathiriwa watapokea ujumbe kupitia barua pepe za kampuni hiyo na wale ambao ajira zao zitaathiriwa watapokea ujumbe kupitia barua pepe zao binafsi.
.
Taarifa hiyo inakuja baada ya ripoti za habari kwamba mmiliki mpya wa kampuni hiyo Elon Musk alipanga kupunguza nusu ya wafanyakazi kwenye kampuni hiyo.