Back to top

Ubora wa Elimu ya Tanzania wajadiliwa.

24 May 2018
Share


Wataalamu wa sekta  ya elimu kutoka nchi za Afrika, Ulaya na Asia wameitaka Tanzania kuwekeza zaidi katika kujenga uwezo wa mfumo wa elimu nchini ikiwemo uwezo wa walimu,maafisa elimu pamoja na miundombinu ya elimu ili kukabiliana na changamoto ya ubora wa elimu unaosababishwa na ongezeko kubwa la wanafunzi katika ngazi ya shule za msingi na sekondari.

Wakizungumza katika kongamano la kimataifa la kujadili ubora wa elimu nchini, baadhi ya wadau wamesema ujio wa sera ya mpya ya mafunzo ya mwaka 2008 ambayo imetambua elimu ya awali kuwa sehemu ya elimu ya msingi,pamoja na sera ya elimu bure imechangia kushuka kwa ubora wa elimu baada ya wanafunzi wengi kuandikishwa kuliko idadi ya walimu na kusababisha mwalimu mmoja kuwa na wanafunzi hadi 180.

Awali akizungumza kuhusu malengo ya serikali na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu, katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Daktri Leonard Akwilapo amekiri moja ya changamoto kubwa inayoikabili serikali kwa sasa ni ubora wa elimu baada ya mipango ya kuongeza madarasa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.