Back to top

Uchaguzi nchini Nigeria wasogezwa mbele hadi Februari 23.

16 February 2019
Share

Uchaguzi wa urais na ubunge nchini Nigeria uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupelekwa mbele kwa wiki moja ambapo Tume ya uchaguzi nchini humo ilitangaza uamuzi huo saa tano kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura.

Zoezi la upigaji kura lilikuwa lianze majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Nigeria katika vituo zaidi ya laki moja na elfu 20 huku nchi hiyo ikiweka rekodi ambapo jumla ya wagombea 73 wanawania kiti cha urais.

Rais Muhammadu Buhari anawania kuchaguliwa kwa muhula wa pili lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kiongozi mkuu wa upinzani na makamu wa rais wa zamani, Atiku Abubakar.

Hata hivyo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, INEC, Mahmood Yakubu, akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura, amesema kwa ratiba ilivyo, isingewezekana tena kwa uchaguzi huo kufanyika kwa wakati.