Back to top

Uchaguzi Serengeti, Simanjiro na kata 21 kufanyika Desemba 2.

15 October 2018
Share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe mbili Desemba kuwa siku ya Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Simanjiro,Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage amesema fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya  tarehe 28 Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.

Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo mawili (2),Jimbo la Serengeti lililopo Mkoani Mara la Mh.Marwa Ryoba  na Jimbo la Simanjiro la Mh.JAmes Ole Millya baada ya wabunge hao kuhama Chama chao.