Back to top

:Uchimbaji madini wilayani Ulanga mkoani Morogoro wafunguliwa.

15 December 2018
Share

Mgodi wa uchimbaji madini ya aina mbalimbali, yakiwemo ruby na spinal uliyopo katika kijiji cha Epanko wilayani  Ulanga mkoani Morogoro uliozuiliwa na serikali kuendelea na shughuli zozote ndani na nje ya mgodi huo kwa miezi sita mfululizo hadi sasa hatimaye serikali kupitia naibu waziri wa madini Mheshimiwa Dotto Biteko ameruhusu uchimbaji huo kuendelea kwa masharti yakulipa fedha walizokuwa wakidaiwa kuibia serikali.


Akizungumza na wachimbaji, wananchi na uongozi wa wilaya ya ulanga naibu waziri Biteko amesema serikali chini ya uongozi wa rais Daktari John Pombe Magufuli haitaruhusu kuona madini yanafaidisha baadhi ya watu huku akiwatahadharisha watu wachache wanaokwamisha kuendelea kwa shughuli za mwekezaji wa kampuni ya tanzgrafite inayo kusudia, uwekezaji mkubwa katika kijiji cha Epanko.


Kwaupande wao wachimbaji katika mgodi huo wameshukuru kufunguliwa kwa shuhuli za uchimbaji huo huku mkuu wa wilaya ya Ulanga Bi.Ngollo Malenya akimhakikishia naibu waziri kusimamia madeni hayo ndipo shuhuli za uchimbaji ziendelee.


Aidha naibu waziri Biteko amezindua rasmi ofisi ya meneja wa madini wilayani humo kufuatia shuhuli za madini katika wilaya hiyo kutokwenda vizuri kufuatia kukosekana kwa usimamizi wa madini wilayani humo huku mbunge wa jimbo hilo Godlack Mlinga akitumia nafasi hiyo kumueleza naibu waziri changamoto ya ukwamaji wa miradi ya maendeleo.