Back to top

Ufisadi wa Fedha ukarabati wa majengo ya chuo Musoma.

22 July 2018
Share

Naibu waziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile,amebaini ufisadi wa zaidi ya shilingi milioni mia tano ambazo zilitolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya chuo cha waganga wasaidizi cha mjini Musoma mkoani Mara.

Kiongozi huyo ambaya amefika katika chuo hicho kwa lengo la kuzindua majengo hayo ambayo yamekarabatiwa,lakini baada ya kubaini kazi hiyo imefanyika chini ya kiwango, amekataa kufanya  uzinduzi huo  nakuagiza wahusika wote wachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akiwa katika wilaya ya Tarime katika mkutano wake na wazee wa mila na wakiwemo Mangariba,naibu  wiziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile,ameviagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali,baadhi ya wazazi wanaoshirikiana na Mangariba kuwakeketa watoto wachanga.

Naye  katibu wa baraza la mila la koo kumi na mbili za wilaya ya Tarime Bw. Mwita Nyasibora,amepongeza juhudi za serikali zikiwemo asasi za jukwaa la utu wa mtoto la Masanga FGM,kwa kufanikiwa kutoa elimu juu madhara ya vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike,hatua ambayo amesema imewezesha wazee wote wa koo hizo kukubaliana kwa kauli moja kuachana na vitendo hivyo.