Back to top

Ufuta kuuzwa kwa njia ya mnada mkoani Lindi.

24 May 2018
Share

Mapendekezo yaliyotolewa na Wenyeviti wa Halmashauri sita za wilaya za mkoa wa Lindi kupinga  zao la ufuta kuingizwa kwenye mfumo wa stakabadhi mazao ghalani,serikali mkoani humo imeridhia mapendekezo hayo na kwamba kwa sasa imeunda taratibu mpya za ununuzi wa ufuta kwa msimu wa mwaka huu wa 2018/2019 kwa njia ya mnada.

Akizungumza na ITV mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kupokea taarifa ya kamati liyoundwa na mkuu wa mkoa wa Lindi,kupitia mapendekezo ya wanyeviti hao,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Abubakari Mjaka, amesema mfumo huo mpya waliupendekeza unaendana na zao la ufuta ambao utamlinda mkulima.

Akitangaza bei dira ya zao la futa  msimu huu wa mwaka 2018/2019,Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amewataka wakulima wa zao la ufuta mkoani hapa kutokubali kuibiwa na wanunuzi wanaotumia chomachoma.