Back to top

Uganda shule,vyuo vyafungwa, harusi,unywaji pombe hadharani marufuku.

18 March 2020
Share

Rais wa Uganda Yoweri  Museveni ameagiza shule zote, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu kusitisha shughuli za masomo kufikia tarehe 28 mwezi huu, kwa mwezi mmoja,ikiwa ni moja ya mikakati ya kujikinga na maambukizi ya homa ya Corona.

Rais Museveni pia amepiga marufuku makongamano ya yote ya kidini,mikutano ya kisiasa, harusi na unyawaji wa pombe hadharani umepigwa marufuku kwa siku 32.

Raia wa Uganda waliokwama maeneo yaliyoathirika na homa hiyo wamepewa fursa ya kurejea nyumbani na kutengwa kwa siku 14 hadi vipimo vya maabara vitapothibitisha kuwa wako salama na waajiri wote nchini humo wameshauriwa kuweka vifaa vya kujikinga na kirusi Corona katika maeneo ya kazi.

Mikusanyiko ya mazishi yamepigwa marufuku,familia ya marehemu itaruhusiwa kuendesha zoezi hilo isipokuwa kwa mgonjwa aliyefariki na Corona serikali itasimamia mazishi hayo na itazika kwa mfumo wa kisayansi pasipo mkusanyiko wa la kifamilia.