Back to top

Ugonjwa wa ‘Ubwiliunga’ wawatesa wakulima wa korosho Nzega.

21 July 2020
Share

Wakulima wa zao la Tumbaku katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamesema licha ya kuhamasika kulima zao la korosho ugonjwa wa ‘Ubwiliunga’ umeonyesha kukwamisha ukuaji wa mikorosho, na  kutupia lawama maafisa Ugani wa wilaya hiyo.

Wakizungumza na kamera ya ITV baadhi ya wakulima wamesema kwa sasa zao la korosho ndiyo tegemeo,  kutokana na zao la tumbaku soko lake kuyumba.

Kwa upande wao maafisa kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele licha ya kutoa elimu  wametaka maafisa Ugani kutembelea mashamba ya wakulima.