Kamishna wa uhamiaji nchini kamishna Generali Dkt. Anna Makakala amesema idara yake imejipanga kuweka Boti za kisasa katika mipaka inayotumia maji kutengenisha Tanzania na nchi nyingine ikiwemo ziwa Nyasa ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu.
Ameyasema hayo baada ya kutembelea kituo cha uhamiaji cha Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na kutembelea mpaka wa Tanzania na Malawi wa ziwa Nyasa ambapo amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Ruvuma.
Awali afisa uhamiaji wa wilaya ya Nyasa mrakibu msaidizi wa uhamiaji wa wilaya ya Nyasa Kibuga Dominick amesema kuwa katika ziwa Nyasa wahamiaji haramu wamekuwa wakitumia ziwa Nyasa kama mlango wa kutokea kuelekea nchi mbali mbali ambapo mwaka huu wamekamata wahamiaji haramu 15 huku wasafirishji wa wahamiaji hao wakitelekeza boti waliyotumia kusafirisha wahamiaji na madumu mawili ya mafuta.