Back to top

Uhusiano mbaya wasababisha shule kuchomwa moto Njombe.

21 October 2018
Share

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopha Ole Sendeka amesema  viashiria vya awali vinaonyesha kuwa mahusiano mabaya kati ya uongozi wa shule na wanafunzi umechangia kuchomwa moto kwa mabweni ya shule ya sekondari Kidegembye mkoani humo.


Tukio la kuchomwa moto kwa shule hiyo limetokea wakati wanafunzi wakiwa hawapo ndani ya mabweni na hivyo kusababisha hasara kubwa za vifaa vya wanafunzi pamoja na vitanda.


Mbunge wa jimbo la Lupembe, Joram Hongoli amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha bweni jipya linajengwa na wanafunzi kuendelea na masomo haraka iwezekanavyo.