Back to top

Uingereza yakataa kuitisha kikao kujadili Brexit.

20 August 2019
Share


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amekataa wazo la kuitisha kikao cha bunge cha dharura kujadili suala la nchi hiyo kujiondoa Umoja wa Ulaya, maarufu kama Brexit, wakati huu wabunge wakiwa katika mapumziko ya majira ya kiangazi.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy Corby, ametoa wito huo baada ya kuvuja kwa ripoti ya serikali inayotahadharisha juu ya kutokea uhaba wa chakula na dawa nchini Uingereza ikiwa nchi hiyo itajiondoa Umoja wa Ulaya bila ya mkataba tarehe 31 mwezi Oktoba.