Back to top

Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania na DRC kuzuia Corona.

22 January 2021
Share

Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

Katazo hilo linaanza leo Januari 22 Januari, ambapo wasafiri wote hawataruhusiwa kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili.

"Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri," amesema Grant Shapps, waziri wa usafirishaji nchini Uingereza.