Back to top

Uingereza yatoa bilioni 307 kuunga mkono serikali ya awamu ya tano

10 August 2018
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Bi. Penny Mordaunt Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo akisema serikali yake imetoa msaada wa shilingi bilioni 307 kwa ajili ya kuunga mkono utekelezaji wa vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli