Back to top

Ujenzi bomba la mafuta Hoima Tanga kuzalisha ajira zaidi ya 10,000

13 September 2020
Share

Rais Dkt.John Magufuli wa Tanzania na Rais wa Uganda Yoweri Mseveni pamoja na Mawaziri wa Nishati wa nchi hizo wamesaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta pamoja na kusudio la kuanza kwa ujenzi wa mradi huo kutoka Hoima Uganda hadi katika kijiji cha Chongoleani mkoani Tanga Tanzania na kueleza faida za mradi huo kwa Watanzania.

Katika kikao kilicho fanyika katika uwanja wa ndege wa CHATO Rais Dkt.John Pombe Magufuli alitumia nafasi hiyo kuwaeleza Watanzania faida za uwepo wa mradi huo kwa watanzania ikiwemo ajira, malipo ya fidia pamoja na masuala mengine muhimu kwa uchumi wa Watanzania pamoja na na wananchi wa Uganda.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema serikali ya Uganda imeridhika na makubaliano hayo ikiwemo mgao wa asilimia sitini ya faidia ya mradi huo kwa Tanzania na arobaini kwa Uganda kama walivyo kubaliana katika mazungumzo yao.

Kabla ya kusini mikataba hiyo Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani na Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania Adeladus Kilangi  wamesema mkataba huo umepitia hatua za kisheria kabla ya makubaliano hayo kufanywa leo na marais wote wawili na wananchi kushuhudia makubaliano hayo.