Back to top

Ujenzi vyuo vya VETA nchini, wasimamizi mtegoni.

21 January 2021
Share

Serikali imewaagiza wasimamizi wote wa miradi ya ujenzi wa vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 25 nchini, kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Machi 31 mwaka huu na haito Mfumbia macho yeyote atakaye kiuka agizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyuo hivyo Katika wilaya za Bahi na Chemba mkoani Dodoma.

Amesema vyuo Hivyo vinatakiwa vikamilike katika muda huo ili kuruhusu mafunzo Kuanza kwa wakati uliopangwa.