Back to top

Ujenzi wa bandari ndogo ya forodhani Ujiji mjini Kigoma wasitishwa.

14 June 2019
Share

Serikali imesitisha ujenzi wa bandari ndogo ya forodhani Ujiji mjini Kigoma, baada ya kituo cha ITV kurusha malalamiko ya wananchi 37 ambao wanadai hawajalipwa fidia ili kupisha maeneo hayo licha ya kufanyiwa tathmini mapema mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga amesema serikali imesikia kilio chao na ujenzi unasimama mpaka wananchi watakapolipwa fidia wiki ijayo.

Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu kwa kina.