Back to top

Ujenzi wa daraja jipya la mto Wami waiva.

09 November 2018
Share

Serikali imesema imekamilisha taratibu zote za ujenzi wa daraja jipya katika eneo la mto Wami ili kurahisisha usafiri kwa watumiaji wa daraja hilo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa ameliambia bunge kuwa daraja hilo jipya litakuwa karibu na lile la sasa na litakuwa refu na pana zaidi kuliko la sasa.

Amesema mkandarasi amepatikana na mkataba umesainiwa, hivyo kinachosubiriwa ni mkandarasi huyo kuingia eneo la mradi kuanza ujenzi huo.

Mheshimiwa Kwandikwa alikuwa akijibu swali la mbunge wa Hai Mhe.Freeman Mbowe lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Rombo Mhe.Joseph Selasini.