Back to top

Ujenzi wa Meli Mwanza, JPM atoa siku 5 wizara ya Ujenzi kukamilisha.

16 July 2019
Share

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametoa siku tano kuanzia leo kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli na vifaa vya ukarabati wa meli vilivyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na mchakato wa kikodi vinafikishwa katika Bandari ya Mwanza.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Bandari ya Mwanza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli tano na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria yanayofanywa na kampuni mbili kutoka Jamhuri ya Korea kwa gharama ya Shilingi bilioni 152 kwa ajili hiyo.

Akiwa bandarini hapo, Rais Magufuli ameeleza kutofurahishwa na ucheleweshaji wa karibu mwezi mmoja wa makontena 58 yenye vifaa vya ujenzi vilivyoagizwa na kampuni za ukandarasi za Kore a Total Marine Innovation na STX JV SAEKYUNG Construction Ltd za Korea kwa sababu ya kusubiri msamaha wa kodi na amemtaka mkandarasi huyo aache visingizio.

Meneja wa mradi wa ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli Mhandisi Abel Gwanafyo amesema ujenzi wa chelezo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Victoria na Mv. Butiama umepangwa kukamilika Machi mwakani .