Back to top

UJERUMANI YATETA NA MAAFISA WA UKRAINE KUJIKINGA NA MASHAMBULIZI

26 October 2022
Share

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, amefanya mazungumzo na maafisa wa Ukraine katika sehemu maalum ya kujikinga na mashambulizi ya anga katika mji wa kaskazini mashariki mwa Kiev.

Punde tu alipowasili katika mji wa Koryukivka, tahadhari ya shambulio la anga ilitolewa na kuwalazimu Rais Steinmeier, Meya Ratan Akhmedov na kundi la wananchi kujificha.

Steinmeier amesema walilazimika kujificha kwa takribani saa moja na nusu katika sehemu hiyo maalum na kwamba hali hiyo imetoa taswira ya jinsi mazingira yalivyo kwa watu wanaoishi nchini humo.

Kulingana na jeshi la anga la Ukraine, tahadhari hiyo ilitolewa baada ya jeshi la Urusi kurusha katika nchi jirani ya Belarusy, ndege 10 zisizokuwa na rubani zilizoundwa nchini Iran.