
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenksy, ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kufidia nakisi ya bajeti ya dola bilioni 38 mwaka ujao kwa nchi yake iliyokumbwa na vita baada ya nchi hiyo kuathirika vibaya kiuchumi kufuatia uvamizi wa Urusi.
Katika mkutano wa kimataifa wa kujadili ujenzi mpya wa Ukraine mjini Berlin, Zelenksy amewataka viongozi wa Ulaya kutoa msaada mkubwa wa kifedha kwa nchi yake.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa kuijenga upya Ukraine itakuwa kazi ya muda mrefu ambayo lazima ianze mara moja licha ya kuendelea na mashambulizi ya Urusi nchini humo.
