Back to top

Umoja wa Mataifa wazindua mfumo maalum kuwabana wapotoshaji Covid-19

22 May 2020
Share


Umoja wa mataifa umezindua mpango wa kukabiliana na ongezeko kubwa la utoaji wa taarifa potofu kuhusu Ugonjwa wa virusi vya corona kwa kuongeza kasi na ufikishaji taarifa sahihi.

Akitangaza mpango huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres amesema jamii haipaswi kuwafumbia macho viongozi wanaotoa taarifa potofu na wanaoeneza hofu na chuki.

Amesema upotoshaji unaenezwa kwa jumbe mbalimbali baina ya watu kupitia mitandao ya kijamii ambazo waandaaji hutumia njia rasmi kutengeneza na kuzisambaza.

Bwana Guterres amesema ili kukabiliana na hali hiyo,wataalamu wa afya na asasi kama Umoja wa Mataifa zinapaswa kuwafikia watu kwa taarifa sahihi zenye kuaminika.

Katibu Mkuu amesema katika mkakati huo mpya Idara ya Mawasiliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa itatoa taarifa katika dhima kuu tatu.

Amezitaja dhima hizo kuwa ni sayansi ili kuokoa uhai, mshikamano ili kuhamasisha ushirikiano wa ndani na kimataifa na suluhu ili kuisaidia jamii iliyofikiwa.