Back to top

Unywaji wa maziwa ni wastani wa lita 49 kwa mwaka kwa mtu mmoja.

19 September 2019
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina amesema serikali imedhamiria kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 2.7 kwa mwaka za sasa na kufikia lita bilioni 7 ifikapo 2020 itakayokwenda sambamba na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za maziwa na unyweshaji wa maziwa kwa watoto katika shule za msingi.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati akizungumzia siku ya unywaji maziwa septemba 25 mjini Iringa, ambapo amesema kwa sasa unywaji wa maziwa ni wastani wa lita 49 kwa mwaka kwa mtu mmoja badala ya lita 200 zinazoelekezwa na shirika la afya duniani (WHO).