Back to top

Uongozi kiwanda cha Dangote wasema hakina mpango wa kufunga kiwanda.

16 February 2021
Share

Uongozi wa kiwanda cha Dangote mkoani Mtwara umekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai uongozi huo unampango wa kufunga kiwanda.  

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Abdullahi Babu alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya taarifa hizo zinazosambaa mitandaoni huku zingine zikidai kwamba kiwanda hicho kitasimamisha kazi wafanyakazi wake na kufunga kiwanda hicho, ambapo amesema kiwanda hicho uzalishaji wake unaendelea vizuri. 

Pamoja na hayo Bwana Babu ameeleza kuwa kiwanda hicho kina ushirikiano mzuri na serikali na tangu kimeanza kutumia gesi kuzalisha saruji kwani uzalushaji umeongezeka na ufanisi wa kazi umeonekana. 

Amewataka Watanzania kupuuza taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa na watu wasio wema kwa lengo la kuchafua taswira nzuri ya kiwanda hicho.