Back to top

Ushirikiano utaondoa wimbi la uhamiaji haramu

20 July 2018
Share

Kamishna wa idara ya uhamiaji nchini Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala ametembelea  kituo cha uhamiaji cha Congresso  mkoani Lichinga nchini Msumbiji na kusema ushirikiano baina ya  maafisa uhamiaji wa Msumbiji na Tanzania utasaidia kuondoa  changamoto ya wahamiaji  haramu.

Akizungumza  na maofisa uhamiaji wa  Msumbiji  Kamishna  wa uhamiaji  Generali Dkt. Anna Makakala  amesema kuwa ushirikiano wa idara ya uhamiaji ya Tanzania na Msumbiji utasaidia kudhibiti wahamiaji haramu wanaotumia kuvuka  maeneo yasiyo rasmi maarufu kama vipenyo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme amebainisha changamoto katika idara ya uhamiaji mkoani humo ikiwemo ubovu wa magari.

Mbali na kutembelea nchini Msumbiji katika ziara yake mkoani Ruvuma Kamishna Jenerali wa uhamiaji Dkt. Makakala ametembelea vituo vya uhamiaji vya Tunduru,Ruvuma,Mbinga na Mkenda  mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.