Back to top

Vifo kutokana na virusi vya Corona vyafikia 2,707

25 February 2020
Share

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na Virusi vya Corona imeshafikia 2,707 huku walioambukiza mpaka sasa ikionesha wameshafikia 80,328.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Worldometers unaofuatilia matukio yanayotokea duniani kwa kila sekunde umeeleza kwamba watu ambao afya zao zimeshaanza kuimarika kutokana na virusi hivyo vya Corona mpaka sasa imefikia 27,814. 

Wakati huo huo Mlipuko wa virusi vya homa ya Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa masoko ya fedha hatua ambayo imesababisha wawekezaji kukimbilia kuuza mali zao zilizo kwenye hatari kama vile hisa zisizo na riba ya kudumu kutokana na wasiwasi juu ya athari za kiuchumi kufuatia virusi vya Corona.

Jijini Tokyo, kipimo cha wastani cha Nikkei kilishuka kwa zaidi ya alama 1,000 mara tu baada ya kufunguliwa leo Jumanne na Kiwango hicho kilikuwa ni kwa zaidi ya asilimia nne.