Back to top

Vijana washauriwa kupima vinasaba kabla ya kuanzisha mahusiano.

19 June 2020
Share

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema Tanzania imetajwa kuwa nchi ya nne yenye wagonjwa wengi wa sickle cell (Selimundu) duniani ambapo asilimia saba ya wagonjwa hao hufariki kila mwaka huku wengi wao wakiwa ni watoto wadogo.

19 June kila mwaka dunia hutumia siku hii kuadhimisha siku ya sikoseli ulimwenguni huku kauli mbiu ya mwaka huu kwa hapa nchini ikisema “Huduma bora kwa kila muhitaji chukua hatua panua wigo”.

Waziri Ummy amewataka vijana kabla ya kuanzisha mahusiano kupima vinasaba vya ugonjwa huo ili kupunguza idadi ya watoto wenye ugonjwa.
 
Nae Dkt Deogratius Soka Mkurugenzi wa shirikisho la wadau wa sikoseli amewataka wazazi mara baada ya kujifungua kuwapima watoto ili kugundua kama wana ugonjwa huo au  hawana.