Back to top

Vijiji vinavyowaficha waganga wa kienyeji kuwekwa chini ya ulinzi.

23 January 2021
Share

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wanagabo amemuagiza kamanda wa Jeshi la Polisi mkoai humo Jastine Masejo kuviweka chini ya ulinzi mkali  vijiji vyote vinatakavyo bainika kuwaficha na kuwahifadhi waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba ambao wamekuwa wakiwadhulumu wananchi kwa watoza fedha na kufanya ramli chonganishi.
 
Hatua hiyo inakuja baada ya kujitokeza malalamiko kutoka kwa wananchi na madiwani katika wilaya ya Sumbawanga juu ya lambalamba hao kuwa kikwazo kutokana na kuwadhulumu fedha pamoja na kusababisha mogongano katika familia.

Awali akiongea na wananchi kuzunguka vijiji tofauti mkoani hapa mkuu wa mkoa wa Rukwa ameligiza jeshi la polis kuvifungia ndani  vijiji au kijiji ambacho kitabainika kuwahifadhi lambalamba.