Back to top

Viongozi wa dini waeleza wanavyopigwa na wazee wa mila mkoani Mara

04 January 2020
Share

Vita dhidi ya ukeketaji na tohara isiyosalama katika mkoa wa Mara bado inaonekana kuwa ngumu kutokomezwa  kutokana na misimamo mikali inayoonyeshwa na wazee wa mila kuwa hawako tayari kushusha visu mpaka wototo wote waliokimbia wakeketwe hali inayopelekea viongozi wa dini na wadau wengine wanaopinga mila hiyo kupigwa,na kuuawa  huku wanasisasa na baadhi ya viongozi wa serikali  wakitamka hadharani kuunga mkono suala hilo licha yakuwa lina madhara na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Wakizungumza wakati wa  sherehe za kufunga kambi okozi ya wasichana zaidi ya 500 waliokimbia kukeketwa kutoka majumbani kwao na kwenda kituo cha Masanga kinachofanya kazi na shirika la wadau mbalimbali  wakiwamo viongozi wa dini wameeleza namna ilivyo ngumu kutokomeza suala hilo kama serikali haitatilia mkazo huku wakisimulia maswahibu yanayowapata pale wanapoonekana wakipinga mila hiyo kutoka kwa wazee wa mila.

Wakati kipigo na vitisho vikiendelea kutoka kwa viongozi wa dini,mashirika na watumishi wa umma hivi karibuni naibu  waziri TAMISEMI Mhe.Mwita  Waitara akiwa jimboni kwake alionekana akiunga mkono suala hilo jambo lililoibua taharuki na mshangao kwa wadau wanaopinga mila hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Butiama Anarose Nyamubi  ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima,  amekiri kuwepo kwa changamoto huku akismulia mkasa wa kiongozi mmoja ambaye hakumtaja jina  alivyokuwa akitekeleza mila hiyo.