Kamishna mkuu wa uhamiaji nchini Dkt Anna Makakala amesema kuna changamoto kubwa ya visiwa kutumika kama njia kuu ya kuingia nchini kwa wahamiaji haramu.
Kamshina Makakala ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari baada ya ziara ya siku mbili Zanzibar, kuangalia changamoto mbali mbali zinazokabili sekta ya uhamaiji nchini kwa upande wa Zanzibar.