Back to top

Vitisho vya Iran havijaifurahisha Marekani.

11 June 2019
Share

Marekani imesema haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano na mwenzake wa Ujerumani Heiko Maas mjini Tehran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani amesema kuwa Iran inachagua moja rahisi tu, ijionyeshe kuwa nchi ya kawaida au ishuhudie uchumi wake ukisambaratika. 

Zarif aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie kuwa salama. 

Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana wakati wa ziara yake nchini humo. 

Maas amesema Ujerumani itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mvutano hauongezeki kati ya Marekani na Iran.