Back to top

Vyuo vya maendeleo ya jamii vitumike kutatua tatizo la ajira

28 May 2020
Share

Waziri wa  nchi ofisi ya waziri mkuu,sera,ajira,bunge na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameagiza vyuo vya maendeleo ya jamii nchini vitumike kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kufundisha vijana watakaojiajiri na kuajiri wenzao.

Mheshimiwa Jenista Mhagama ameyasema hayo baada ya kutembelea chuo cha maendeleo ya jamii  (FDC) cha Muhukuru wilayani Songea mkoani Ruvuma  kilichoko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
 
Kwa upande wake kaimu mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Muhukuru Bw.Aisaria Kimambo amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 400 kujenga karakana tano zikiwemo za Useremala na Uashi na pia Septemba 2019 serikali ilitoa zaidi ya shilingi milioni 200 kujenga jengo la utawala na bweni la wasichana.
 
Pamoja na mafanikio ya chuo hicho bw. Kimambo amesema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi changamoto ambazo Mheshimiwa Mhagama ameahidi kuzishughulikia.