Back to top

Wabunge wa CHADEMA wanahesabika kama watoro-Spika Ndugai.

06 May 2020
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amewataka wabunge wa CHADEMA  ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini  watambue wanachofanya ni kinyume na sheria na kuna masuala wanatakiwa kufanya ili waruhusiwe kuingia bungeni humo.

Spika  Ndugai ameliambia bunge kuwa wabunge hao wanahesabika kama watoro,wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni sambamba na kuwa na vipimo vikithibitisha wapo salama dhidi  ya ugonjwa wa virusi vya corona.