Back to top

Wabunge wa EALA wazungumzia maandalizi ya mkutano wa wakuu wa EAC

19 February 2020
Share

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limepokea muswada wa matumizi na mapato ya nyongeza ya Dola za Marekani Milioni 4.8.

Katika kikao hicho, bunge pia limepokea taarifa ya hesabu zilizokaguliwa na Kamisheni ya Ukaguzi ya jumuiya hiyo za mwaka 2017/2018.

Baada ya kikao hicho baadhi ya wabunge wamezungumzia mkutano wa wakuu wa nchi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo unaotarajiwa  kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu.

Katika hatua nyingine baadhi ya wabunge wamemuomba Spika umuhimu wa jumuiya kuangalia uwezekano wa bunge kumuenzi aliyekuwa Rais wa  Kenya, hayati Daniel Arap Moi kwa mchango wake kwa bunge na jumuiya kwa ujumla.