Back to top

Wabunge waitaka serikali kufikisha fedha kwa wakati kwenye miradi.

13 June 2020
Share

BUNGENI DODOMA

Wabunge wamesisitiza umuhimu wa serikali kutoa kwa wakati muafaka fedha zinazopangwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili zikafanye kazi zilizokusudiwa.

Wakichangia bajeti hiyo, baadhi ya wabunge wamesema barabara zikiwemo za vijijini zina hali mbaya hivyo ni vyema zikakarabatiwa mapema ili kuondoa adha kwa wananchi.

Kuhusu sekta ya kilimo, wameitaka serikali iangalie namna ya kuiboresha kwa kuitengea fedha za kutosha kwa kuwa inahusisha Watanzania wengi na wabunge wengine wameitaka serikali iziangalie upya bodi zinazoundwa kusiamia mazao.

Akitoa mchango juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kushindwa kuwalipa watumishi Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.Ruth Mollel ameitaka serikali iwalipe watumishi stahiki zao mapema.