Back to top

Wachimbaji watakaoruka ukuta Mererani kufutiwa vibali vya kufanyakazi.

17 February 2019
Share

Waziri  wa madini Dotto Biteko  amesema kuanzia sasa mchimbaji madini yaTtanzaniate kwenye migodi ya Mererani atakayebainika kuingia au kutoka kwenye eneo hilo kwa kuruka ukuta  atafutiwa leseni au kibali cha kufanyakazi  kwenye migodi hiyo na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. 

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mererani katika ziara yake inayoendelea ya kukagua miundombinu ambapo pia alizindua  uwekaji wa mitambo ya kisasa ya usalama kwenye  uzio wa kuzunguka migodi hiyo  jengo  la wanunuzi wa madini na kituo cha pamoja.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya  kudumu ya madini Danstan Kitandula anasema serikali imeonesha ni ya kuboresha sekta ya madini na kamati yake itahakikisha  miswada yenye maslahi kwa umma inafanyiwa kazi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti anasema serikali ya mkoa itatekeleza maagizo yote yenye lengo la kkuboresha ufanisi na kuchukua hatua kwa watakaokiuka taratibu