Back to top

Wachimbaji watakiwa kuchukua tahathari ya matumizi ya Zebaki.

16 February 2020
Share

Wataalam wa madini wamewashauri wachimbaji wadogo migodini kuchukua tahadhari juu ya matumizi ya Zebaki ili kujikinga na madhara ya  afya yanayoweza kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu wa viungo.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Uchimbaji Mdogo Tanzania, Bibi Theonestina Mwasha, ametoa ushauri huo kwa wachimbaji wadogo wa migodi Wilaya za  Geita na Chato, kufuatia migodi mingi ya wachimbaji wadogo kuendelea kutumia Zebaki kukamatia dhahabu.

Baadhi ya wamiliki wa migodi ya wachimbaji wadogo wakaeleza sababu za kuendelea kutumia Zebaki wakati wa uchenjuaji wa dhahabu ni upatikanaji wake licha ya kemikali hiyo kufahamika kwa kiwango kikubwa kwamba ihatarisha maisha ya binadamu.

Ukosefu wa vifaa kinga na mazingira hatarishi katika maeneo ya migodi ya wachimbaji wadogo ni suala ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wadau wa sekta hiyo.