Back to top

Wadau wa elimu Mtwara wachangia Milioni 185 ujenzi wa madarasa

23 June 2018
Share

Wadau wa elimu mkoani Mtwara wamechangia shilingi milioni 185 za kujenga vyumba vya madarasa 48, katika shule 10 za msingi za halmashauri ya wilaya ya Mtwara, ambazo wanafunzi wake walikuwa wakisoma chini ya Mikorosho, huku agizo likitolewa ujenzi wa madarasa, hayo uzingatie ubora.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Gaspa Byakanwa alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo, kwenye shule 5 kati ya hizo 10, ambapo amesema, pamoja na uharaka wa ujenzi wa madarasa hayo, ili wanafunzi waondokane na adha ya kusoma chini ya mikorosho, serikali haitakubalika kuona madarasa hayo yakijengwa chini ya kiwango.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi, mbali na kuwashukuru wadau wa elimu kwa michango waliotoa na wao kuahidi kutumia nguvu zao kuchangia maendeleo, wameomba shule hizo zipatiwe umeme ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.