Back to top

Wadau wa elimu wajitokeza kusaidia wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

19 July 2018
Share

Wadau wa elimu wilayani Kahama wameanza kutekeleza agizo la serikali la kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujifunza zaidi masomo ya Sayansi lengo likiwa ni kuisaidia serikali kupata wataalamu wengi zaidi, nchi inapoelekea katika uchumi wa kati kiviwanda.

Akiongea wakati akikabidhi Komputer 30 katika baadhi ya shule  za msingi na sekondari wilayani Kahama naibu waziri wa ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa amewashauri wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia vifaa vya masomo ya sayansi katika mashule hali ambayo ameitaja kuwa itasaidia kuwashawishi wanafunzi kusoma masomo hayo na kupata wataalamu wengi zaidi.

Baadhi ya walimu wa shule zilizofanikiwa kupata mgao wa komputer hizo wamesema hali hiyo itaongeza hamasa kwa wanafunzi kujiunga na masomo ya sayansi na kufaulu vizuri kwakuwa awali hakukuwa na vifaa vya kujifunzia.

Baadhi ya wazazi walioshiriki katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo wamesema wako tayari kushirikiana na wadau kuziwezesha shule vifaa vya masomo ya sayansi na kuwashukuru wada umbao tayari wameshaanza kufungua njia hiyo.