Back to top

Wadau wa soka walalamikia ubovu wa viwanja Iringa

21 June 2018
Share

Baadhi ya wadau wa soka mjini Iringa wamelalamikia uhaba wa viwanja vya soka mjini humo huku wakiiomba serikali kupitia halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutazama uwezekano wa kufanyia ukarabati wa viwanja vichache vilivyopo ili viweze kusaidia kukuza mchezo huo katika Manispaa hiyo na mkoa kwa ujumla.

Wakizungumza kwenye mchezo uliozikutanisha timu za Iringa Football Academy dhidi ya Galilaya FC kwenye mzungunguko wa kwanza wa michuano ya soka ya Iringa Challenge Cup ambapo Galilaya FC ililala kwa bao tano kwa bila wadau hao wamesema.

Ubovu huo wa viwanja umeonekana kuathiri mwenendo wa michuano ya Iringa Challenge Cup iliyo chini ya udhamini wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kiasi cha kuzusha malalamiko toka kwa baadhi ya washiriki wa michuano hiyo.

Fredy Mgunda ni Mratibu wa Mashindano hayo anaeleza changamoto wanayoipata katika kuendesha mashindano hayo maarufu Ritta Kabati Challenge Cup licha ya mashindano yenyewe kuleta hamasa na mvuto kwa mashabiki na timu zinazoshiriki.